Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makalla aahidi matumizi sahihi fedha za IMF

Mmmm.jpeg Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa DSM.

Sat, 16 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amemuhakikishia Rais Samia Suluhu kuwa kiasi Cha fedha kitakacholetwa kwenye Mkoa huo kupitia fedha za IMF kwa ajili ya mapambano dhidi ya Covid 19 kitatumika kwa kazi iliyokusudiwa pasipo ubadhirifu

Akizungumza kwenye kikao kazi na Watendaji wa Wilaya za Mkoa huo, amesema tayari zimeundwa Kamati makini zenye wajumbe waadilifu na wachapa kazi watakaosimamia matumizi sahihi ya fedha hizo.

Aidha Kamati hizo zitasimamia hatua kwa hatua Miradi ya Ujenzi wa madarasa, maji na maboresho ya mazingira ya Machinga Jijini humo.

Pamoja na hayo Makalla amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na njema anayoifanya Katika kuwapatia Wananchi huduma Bora na utekelezaji wa Miradi mingi na mikubwa ya Maendeleo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live