Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makalla: Wanaopangisha Magomeni kota ni matapeli

Makazzi Makalla Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amezihakikishia Kaya 644 wakazi wa Magomeni Kota kuwa Serikali itawapatia makazi watu wote wanaostahili na walioainishwa tokea awali.

RC Makalla amesema hayo wakati alipofanya ziara ya Kujiridhisha na kukagua maendeleo ya Mradi huo Wenye thamani ya Sh52.1 bilioni ambapo kwa Sasa Ujenzi huo umefikia asilimia 99.

Ujenzi huo utanufaisha watu zaidi ya 3,000 kutoka Kaya 644.

Aidha Makalla amesema Mradi utakapokamilika Wakazi husika wataitwa na kutangaziwa tarehe rasmi ya kuingia Katika nyumba hizo.

RC Makalla ametoa wito kwa Wakala wa Majengo (TBA) kutumia eneo lililobaki kimkakati kwa kujenga Majengo ya Gorofa ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa Ardhi.

Mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi ya waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota ulianza October mosi 2016 ukihusisha Ujenzi wa Majengo matano yenye gorofa nane hadi tisa ambapo ukikamilika wanufaika wataishi Bure ndani ya Nyumba hizo kwa kipindi Cha miaka mitano

Chanzo: Mwananchi