Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Makalla: Hakuna shule iliyouzwa Kurasini

30c3cc58 0574 41f1 A322 238bdd5469c8 1080x640.jpeg RC amevunja ukimya juu ya taarifa za mitandaoni

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amemaliza hali ya taharuki juu ya uvumi wa taarifa zilizodaiwa kuwa eneo la Shule ya Sekondari Kurasini linauzwa kwa Mwekezaji ambapo amethibitisha kuwa eneo Hilo haliuzwi.

RC Makalla amesema ni kweli kuwa mwekezaji alituma maombi ya kupatiwa eneo Hilo la shule na kuahidi kujenga shule nyingine eneo la mbagala lakini Serikali haikuridhia ombi hilo.

Amesema hayo katika kilichojumuisha Kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya ya Temeke, Baraza la Madiwani, Viongozi wa CCM Wilaya, RC Makalla amesema mchakato wa kuuza Eneo la Shule sio rahisi kwakuwa ni lazima Maombi yaanze ngazi ya Kata, Wilaya, Mkoa Kisha Mkoa upeleke Wizarani na Wizara iwasilishe ngazi ya juu.

RC Makalla amesema amejiridhisha pasipokuwa na shaka kuwa eneo Hilo haliuzwi na Halmashauri haina uwezo wa kufanya mauzo ya namna hiyo.

Aidha RC Makalla amesema kikao hicho pia kimepitia taarifa ya Kamati iliyoundwa kupitia dosari zizojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa fedha za mikopo ya Asilimia 10 ya Halmashauri ya Temeke kwa Vikundi vya ujasiriamali ambapo ametangaza kuunda upya Kamati ya kufuatilia kwa kina suala Hilo ili itoe taarifa sahihi.

Kikao hicho pia kimejadili ajenda ya kufanikisha Zoezi la anuani za Makazi na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 pamoja na mapokezi ya Rais Samia Suluhu Hassan siku ya Jumapil ya February 20.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live