Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewaelekeza TANROAD kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo Cha usalama Barabarani kudhibiti tatizo la ajali Barabara ya Morogoro eneo la Kiluvya kwa Komba Kudhibiti tatizo la ajali eneo hilo kufuatia eneo hilo kushamiri kwa ajali.
Mapema jana asubuhi RC Makalla amefika eneo hilo na kupokelewa na kundi la Wananchi waliokuwa wamejiandaa kulala Katika ya Barabara kuzuia shughuli za usafiri Kama sehemu ya kufikisha ujumbe kwa Serikali.
Akizungumza na Wananchi hao RC Makalla ameonyesha kuchukizwa na TANROAD kupuuza Malalamiko ya Wananchi na maelekezo ya Serikali ambapo August 31 wakati wa zoezi la kusikiliza kero za Wananchi Jimbo la Kibamba hoja hiyo iliibuka na TANROAD kuagizwa kushughulikia kero hiyo lakini mpaka Leo hakuna utekelezaji.
Kutokana na hilo RC Makalla amelazimika kumpigia simu Meneja wa TANROAD na kumtaka kufika eneo la tukio Kuangalia Mpango sahihi wa kudhibiti ajali kwenye eneo hilo.
Aidha RC Makalla ametoa wito kwa Jeshi la Polisi kutoa adhabu Kali kwa Madereva wasiozingatia alama za Barabarani huku akiwataka Madereva kuzingatia Sheria za usalama Barabarani.
Maelezo hayo yamepokelewa na Jeshi la Polisi ambalo limeahidi kusimamia na kutekeleza Maelekezo yote yaliyotolewa na RC Makalla huku likitoa wito kwa Wananchi kuchukuwa tahadhari wawapo barararani.
Kwa mujibu wa wakazi wa Kiluvya kwa Komba, Wananchi wamekuwa wakipoteza maisha kwenye eneo la kivuko Cha watembea kwa miguu Kutokana na baadhi ya Madereva kutoheshimu alama za Barabarani.