Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Mahenge atoa onyo kwa ma DC, DED

Sat, 22 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amegawa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo leo Jumamosi Desemba 22, 2018 kwa wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa huo na kuwataka kufuata taratibu na umakini katika ugawaji kwa wahusika.

Dk Mahenge amesema kunaweza kuwa na mabadiliko kidogo kwenye fomu itakayojazwa na wafanyabiashara lakini kusiongezeke hata shilingi moja kwenye bei elekezi ya Sh20,000.

Vitambulisho 25,000 vimegawiwa ambavyo vitachangia Sh500 milioni kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

"Kwa ajili ya kumbukumbu nzuri ya hesabu ya ukaguzi, tunaweza tukaongeza vitu vidogo katika ugawaji wa vitambulisho hivyo lakini msije mkaongeza gharama nyingine ambazo zitakuwa ni kero kwa wafanyabiashara. Nataka bei ibaki palepale Sh20,000," amesema Mahenge.

Ofisa kutoka TRA, Kabula Mwelezi ametahadharisha wafanyabiashara wote wenye namba ya mlipa kodi kuwa hawatapata vitambulisho hivyo nia ikiwa ni kuwafanya waendelee kulipa kodi.



Chanzo: mwananchi.co.tz