Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kunenge apokea ng'ombe 500 kwa ajili ya Eid Al Adha

RC Kunenge Apokea Ng'ombe 500 Kwa Ajili Ya Eid Al Adha RC Kunenge apokea ng'ombe 500 kwa ajili ya Eid Al Adha

Thu, 29 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge, amepokea Ng'ombe 500 na mbuzi 1,000 kutoka Jumuiya ya IDDEF ya nchini Uturuki wakishirikiana na Rahma Fondation ya Tanzania kwa ajili ya sadaka ya sikukuu ya Eid Al Adha.

Akikabidhi Sadaka hiyo ,Sheh Bahadhir kutoka katika taasisi hiyo, katika machinjio ya Pangani, mjini Kibaha, alisema IDDEF , taasisi ya Rahmah ya nchini Tanzania wametoa ng'ombe na mbuzi hao kwa ajili ya Sadaka hiyo hususan kwa wajane,yatima na wazee.

Aidha aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kukubali msaada huo na kutoa machinjio hiyo kwa ajili ya kuchinjia wanyama hao.

Akipokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa Kunenge, aliishukuru taasisi hizo kwa sadaka hiyo ya ibada ya kuchinjwa ya Eid Al adha na kwamba sadaka hiyo itagawanywa kwa wahitaji ikiwemo, yatima,wajane na wazee.

"Nimepokea Ng'ombe 500 na mbuzi 1,000 Kwa ajili ya sadaka ya ibada ya kuchinjwa ya EId Al Adha naipongeza Jumuiya hii Rahma Foundation na IDDER na mashekh wote kutoka Uturuki kwa kuendelea kushirikiana na nchi yetu katika nyanja mbalimbali"alisema Kunenge.

Licha ya hayo Kunenge alieleza ni vema Sadaka hizo zikatolewa Kwa wahitaji ikiwemo yatima,wajane, wazee, watu wasiojiweza na waalimu wa dini.

Kwa upande wake mwakilishi wa Shekh wa Mkoa wa Pwani, Salimini Buda,aliishukuru taasisi hiyo na kwamba Sadaka hiyo itawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live