Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kunenge: Mtalipwa Fidia

Kunenge Aboubakar Kunenge Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge amekutana na Wananchi wa Vijiji vya Manda na Mkange Chalinze Wilayani Bagamoyo, ambao wanalalamikia kutolipwa Fidia baada ya kuwepo Mchakato wa Ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki, Makurunge, Saadani Tanga.

“Mtalipwa Fidia kama walivyolipwa wenzenu wa Tanga, kwasababu ya Mazingira ya suala lenyewe kwamba Mradi ni mmoja Tathimini ilikwisha fanyika kilichofanya msilipwe kipindi hicho ni kukosekana kwa fedha” alisema Kunenge.

“Nimelichukua tutaenda kushauriana na Wizara fidia zilipwe kupitia vigezo walivyotumia kulipa wananchi wa Vijijini Jirani na kama inavyonekana kwenye Tathimini ya awali. Tutatumia hekima pia kutafutia ufumbuzi suala hilo,vuteni subira suala hili tunalishughulikia”alisisitiza Kunenge

Jambo lilowatia hofu Wananchi hao ni kufanyika kwa Tathimini mpya ambayo fomula iliyotumika ni tofauti na ya mwaka 2019,hivyo kuwepo kwa Tathimini mbili kwenye mradi huo mmoja, na wakati huo huo Wananchi wa Vijiji Jirani wamelipwa kwa Tathimini ya awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live