Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kilimanjaro ataka bei ya sukari ibandikwe madukani

Hii Hapa Bei Elekezi Ya Sukari RC Kilimanjaro ataka bei ya sukari ibandikwe madukani

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha kila duka linalouza sukari linabandika tangazo la bei ya sukari ili mteja ajue bei halisi.

Babu ametoa agizo hilo leo Februari 09, 2024 katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika mkoani hapa.

Amesema hatavumilia kuona wananchi wanaumizwa na wafanyabiashara.

Licha ya Serikali kutoa bei elekezi ya sukari nchini, Kilimanjaro ikiwa Sh2,800 hadi Sh3, 000, wafanyabiashara wameendelea kuuza kilo moja ya kati ya Sh3,500 hadi Sh5,000 kinyume na bei elekezi.

Mwananchi Digital imepita katika baadhi ya maduka ndani ya Manispaa ya Moshi na kushuhudia baadhi ya wafanyabiashara wakiuza sukari kati ya Sh3,500 hadi Sh5, 000 kwa kilo moja.

"Waheshimiwa wakuu wa wilaya, kila mtu ambaye ana duka na anapenda kuuza sukari, lazima aandike tangazo la bei elekezi mbele ya duka lake, Serikali tunaondoa ushuru, tunafanya kila kitu lakini bado wanataka wajinufaishe waumize wananchi, hakuna mtu atakayekubali kwa jambo hili,” amesema Babu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wakazi wa Moshi, wamesema licha ya Serikali kutoa bei elekezi ya sukari wameendelea kuuziwa ile ile inayowaumiza.

Ester Nyalu, mkazi wa Msaranga ameiomba Serikali kuwachukulia hatua wale wanaokiuka maelekezo ya Serikali kwa kuwa wanaumiza watu ambao hawana hatia.

"Asubuhi nimemtuma mwanangu anichukulie sukari kilo moja dukani, nashangaa anauziwa kilo moja ya sukari Sh5,000 wakati Serikali ni Sh2, 800 hadi Sh3, 000 hii bei wanayotuuzia hawa wafanyabiashara inatoka wapi," amesema Nyalu.

Mkazi mwingine, Joshua Joseph amesema tangu Serikali itoe tangazo la kushuka bei ya sukari hajawahi kuona unafuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live