Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kigoma awafunda watumishi kuhusu utoaji takwimu

10374 Takwm+pic TanzaniaWeb

Sun, 1 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emmanuel Maganga amesema Serikali haipo tayari kuwavumilia watumishi mkoani humo watakaohusika kutoa takwimu za uongo kwa lengo la kupotosha ukweli.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Juni 29, 2018 wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja kuhusu hali ya upatikanaji wa takwimu ya viashilia vya mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya kimataifa ya maendeleo endelevu.

Amewataka watumishi kila mmoja katika nafasi yake kutoa takwimu za ukweli bila kupindisha.

Amewataka kutotoa takwimu za uongo kwa ajili ya kuwafurahisha viongozi, badala yake watoe takwimu sahihi zitakazoleta maendeleo katika Mkoa huo.

"Kuna wakati mwingine mmekuwa na tabia ya kudanganya takwimu, mfano kwenye ujio wa viongozi wa ngazi za kitaifa pamoja na mbio za mwenge, mnatoa takwimu za uongo," amesema.

Irenius Ruyobya akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Albina Chuwa, amesema Serikali haimzuii mtu yeyote kufanya tafiti lakini wazingatie taratibu za kitakwimu.

" Sheria ya takwimu inasistiza watu kuzifuata kwani ni tasnia kama tasnia nyingine zina taratibu zake na si kila mtu anaweza kuwa mtakwimu," amesema Ruyobya.

Mwakilishi kutoka Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Rukiya Wadoud amesema upatikanaji wa takwimu sahihi utasaidia kutayarisha mipango na utekelezaji itakayohudumia mahitaji ya watu wa eneo husika.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz