Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kigoma atoa maagizo kwa maafisa utumishi

Rc Kigomaaaaaaaaaa.jpeg RC Kigoma atoa maagizo kwa maafisa utumishi

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewataka maafisa utumishi katika halmashauri mkoani humo kuhakikisha wanawafikia watumishi wa Umma katika maeneo yao ya kazi ili kushughulikia kero zinazowakabili na kuondoa manung'uniko yanayowavunja ari ya utendaji kazi.

Mkuu wa Mkoa ametoa maelekezo hayo alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kakonko akiwa katika ziara ya kikazi iliyolenga kukagua miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero za wanachi katika wilaya hiyo.

"Msiwaache watumishi wakatoka katika vituo vyao vya kazi na kuwafuata ofisini hali inayosababisha kupoteza muda wa kutekeleza majukumu yao, hivyo wekeni ratiba ya kuwafuata na kushughulikia changamoto zao kwani mnafahamu dhamana yenu katika utumishi wa Umma" amesema Andengenye.

Aidha Andengenye amewasisitiza wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanawawezesha maafisa utumishi katika halmashauri zao kuwafikia watumishi kwenye vituo vyao vya kazi kwa ajili ya kutatua changamoto zao.

Kadhalika mkuu wa mkoa amewakumbusha watumishi hao kuzingatia miongozo ya kiutumishi kwa kutokiuka sheria na maadili ya kazi zao.

Kupitia ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa amekagua ujenzi wa miundombinu ya kielimu inayotekelezwa na Serikali kwenye kata ya Nyamtukuza wilayani Kakonko na kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wake.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Kakonko Ndaki Mhuli ameishukuru Serikali kupitia programu ya BOOST imefanikisha kujengwa kwa miundombinu ya kielimu shule ya msingi Nyamtukuza kwa thamani ya Shilingi 361,500,000 pamoja na shule ya msingi Mwilonge kwa Shilingi 110,600,000.

Aidha Ndaki amesema Shilingi Mil. 603,890,562 zinatumika kujenga shule ya sekondari Rutega iliyopo kwenye kata hiyo ambapo ujenzi wake umefikia hatua ya upakaji wa rangi.

"Kwa mwaka wa Masomo 2024 hatutarajii kuwa na changamoto ya ukosefu wa madarasa kwa wanafunzi tunaotarajia kuwapokea kwa ajili ya kuanza kidato cha kwanza" amesema Ndaki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live