Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kigoma afunguka azikataa takwimu mtihani darasa la saba

Mtihani La Saba Wazaziiii.jpeg RC Kigoma afunguka azikataa takwimu mtihani darasa la saba

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, imesema taarifa inayozunguka kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii ikizungumzia kuhusu takwimu za wanafunzi waliofanya mtihani wa sarasa la saba mkoani Kigoma haina ukweli.

Kuanzia jana baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kulikuwa na taarifa inazunguka ikieleza kuwa nusu ya wanafunzi waliotarajiwa kufanya mtihani wa darasa la saba mkoani Kigoma, hawakuweza kufanya mtihani huo kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro.

Taarifa hiyo ilisema wanafunzi 53,000 walifanya mitihani yao kati ya wanafunzi 102,948 waliotarajiwa, lakini leo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma imefafanua kuwa takwimu halisi bado hazijapatikana.

“Kuna taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikieleza kuwa wanafunzi 49, 948, kati ya wanafunzi 102, 948 katika Mkoa wa Kigoma hawakufanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2023.

“Idara ya Elimu Mkoa wa Kigoma inakanusha taarifa hiyo inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa sahihi na taarifa hiyo haikutolewa na Afisa Elimu Mkoa wa Kigoma na wala hakuongea na Mwandishi aliyetoa habari hizo,” imesema taarifa iliyosainiwa na Andrew Mlama, Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma.

Mlama ameitaka jamii kupuuza taarifa kuhusu takwimu hizo na kusisitiza kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inawataka waandisi wa habari wasiandike habari ambazo hazijathibitishwa na mamlaka husika.

Amesema takwimu za waliofanya mtihani na wasiofanya zitatolewa na mamlaka husika mara baada ya mchakato wa ufanyaji mtihani kukamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live