Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kigoma adai madiwani wanakwamisha miradi ya maendeleo

58695 Pic+kigoma

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Mkuu wa Mkoa wa Kigoma,  Brigedia Jenerali mstaafu Emmanuel Maganga amesema baadhi ya madiwani wa halmashauri za  Mkoa huo wanakwamisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Mwi 20, 2019 wakati akifungua kikao cha mafunzo na maelekezo ya maadili kwa viongozi wa umma.

Amesema diwani hapaswi kuleta kampuni yake kwa ajili ya kupewa mradi wa halmashauri husika iliyoletwa na Serikali, akibainisha kuwa hiyo ni sababu ya kukwama kwa miradi.

Amesema miongoni mwa miradi inayokwama ni ya maji ya mwaka 2013 /14, "Madiwani wao ndio walikuwa kwenye kampuni na wanajulikana tunawajua wote ni jambo ambalo liko wazi hakuna sababu ya kumung'unya maneno.”

Kaimu katibu msaidizi wa sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya Magharibi, Gerald Mwakitebele amesema lengo la mafunzo hayo ni kusimamia na kukuza maadili.

“Tupo kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwakumbusha wajibu wa watumishi wa umma maana ndio kazi yetu lengo letu viongozi wawe mfano wa maadili kwa wananchi," amesema Mwakitebele.

Pia Soma

Diwani wa Buhanda,  Aroni Nyabakari amesema kukwama kwa miradi ya maendeleo katika halmashauri inatokana na baadhi ya madiwani kuwa na mgongano wa kimaslahi.

Chanzo: mwananchi.co.tz