Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kigaigai atoa magizo miradi ya Maji Kilimanjaro

MAJII RC Kigaigai atoa magizo miradi ya Maji Kilimanjaro

Tue, 21 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amewataka wakuu wa Wilaya mkoani humo, kusimamia kikamilifu miradi ya maji inayotekelezwa katika maeneo yao na kuhakikisha inakamilika kwa wakati uliopangwa na thamani ya fedha inaonekana.

 Mbali na wakuu wa wilaya pia amewataka wakandarasi kutekeleza miradi hiyo kama walivyotenda na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na viwango vilivyowekwa.

Ametoa agizo hilo leo jumanne Desemba 21, 2021 mjini Moshi katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa, wakati wa utiaji wa saini mikataba 11 ya utekelezaji wa miradi ya maji 19 kati ya 22 iliyotangazwa katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Akitoa taarifa kwa niaba ya Kagaigai, Mkuu wa Wilaya ya Moshi Abasi Kayanda, amesema hawatarajii katika Mkoa wa Kilimanjaro mradi kuvuka miezi 6 au kuonekana madudu.

"Ni jukumu lenu wakuu wa wilaya kwenda kusimamia miradi hii ili itekelezwe katika viwango vinavyokubalika lakini pia wapo mainjinia wa Ruwasa ngazi za Wilaya ni jukumu lao kuona ubora wa kazi zilizofanyika " 

Ameongeza kuwa"Haitopendeza wanakuja viongozi wa kitaifa wanakuja kushuhudia madudu wakati sisi tupo kwenye maeneo haya , tusingependa haya yatokee katika mkoa wetu tunahitaji kila mmoja awe msimamizi katika miradi hii tuone thamani ya fedha kwa kila mradi utakaotekelezwa"

"Tuombe wakandarasi, kazi hii mmeiomba wenyewe sasa nendeni mkaonyeshe utaalamu wenu  na ujuzi wenu katika kutekeleza miradi hii"

 Akitoa taarifa ya utekekezaji wa miradi ya maji Meneja Wakala wa Maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa),Mkoa wa Kilimanjaro, Weransari Munis amesema kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Mkoa huo umetengewa bajeti ya Sh 12.3 kwa ajili ya utekelezaji wa maji vijijini.

Amesema mbali na fedha hizo zilizotengwa kwenye bajeti pia mkoa huo umepokea Sh3.5 bilioni inayotokana na fedha za uviko-19, ambapo itaongeza miradi mipya saba ya maji.

Amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutawanifaisha wananchi 324,797 na hivyo kuongeza huduma ya maji vijijini kutoka asilimia 83 iliyopo kwa sasa hadi kufikia 87.

"Miradi hii ni ile itakayofanyiwa ukarabati, upanuzi na ujenzi na inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi sita, yaani katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha 2021/2022"

Chanzo: www.mwananchi.co.tz