Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Katavi aitaka NFRA kukamilisha ujenzi wa maghala ya chakula mapema

Ghala Katv2.jpeg RC Katavi aitaka NFRA kukamilisha ujenzi wa maghala ya chakula mapema

Wed, 13 May 2020 Chanzo: --

WAKALA wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametekeleza ujenzi wa mradi wa vihenge vya kuhifadhia chakula, maghala na miundombinu kwa asilimia 75 huku mradi huo ukitegemea kukamilika julai 14 mwaka huu.

Akisoma taarifa fupi kuhusu maendeleo ya mradi huo mbele ya Mkuu wa Mkoa na viongozi wengine, Muhandisi Mussa Chiyanda ambaye ni mhandisi mkazi wa mradi katika Manispaa ya Mpanda amesema mradi huo ulianza kujengwa January 14, 2019 huku mradi huo ukigharimu kiasi cha shilingi bilioni 14.

Chiyanda amesema ujenzi huo ukikamilika wananchi watapata fursa ya soko la uhakika kuuza mazao yao kutokana na kuwepo kwa vihenge sita vya kuhifadhi mazao tani 3,333 kila kimoja.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera, amefika kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo nakuwataka kukamilisha haraka ili wananchi waweze kuhifadhi mazao yao katika vihenge hivyo.

"Tumalize mapema kwa sababu kipindi hiki ndio kipindi cha kupokea mazao ambapo NFRA kipindi hiki imepewa kazi ya kununua mazao na kuyatunza,"amesema Homera.

Aidha, Homera amesema, vihenge hivyo vinauwezo wa kutunza tani 28,000 za mazao hivyo wasipoteze muda kwani Mkoa wa Katavi mazao yanawahi kukomaa na tayari mahindi yameanza kununuliwa.

Hata hivyo Homera amewataka wananchi watengeneze mazao yao kwa ubora ili yaweze kuhifadhiwa katika vihenge na yauzike hata nchi zingine sio Tanzania pekee.

Chanzo: --