Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Katavi aelezea vivutio vyenye maajabu, kipo cha kukupandisha cheo

76540 Pic+utalii

Fri, 20 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini nchini Tanzania inaendelea na mikakati ya kutangaza vivutio ili kukuza utalii kama ilivyo katika mikoa ya kaskazini.

Mikakati hiyo ni pamoja na maadhimisho ya utalii yanayofanyika katika viwanja vya Kihesa/ Kilolo, Mjini Iringa vikiwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii.

Akizungumza katika maadhimisho hayo leo Ijumaa Septemba 21,2019 Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera amesema vivutio hivyo vinatakiwa kutangazwa huku akitaka kampuni za utalii kuwekeza kwenye mikoa hiyo.

"Katavi tuna Sokwe wakubwa wanao fanana na sisi wanadamu, nimeshindwa kuja nao kwa sababu wangeweza kunipiga mimi mwenyewe mkuu wa mkoa," amesema Homera.

Amesema pia wana eneo la maji moto ambayo yana sifa ya kuchemsha mayai na yakaiva, lakini pia uwepo wa mti pacha ambayo mtu yoyote ukienda kuomba au kufanya tambiko la kupata watoto basi unapata watoto pacha na maeneo hayo yanaheshimika na ni vivutio vinavyofaa kwa utalii.

"Nawakaribisha mje kunywa haya maji yana baraka ukija unaweza pandishwa cheo mara moja," amesema huku umati wa watu waliokuwapo kwenye maadhimisho hayo wakifurahi

Pia Soma

Advertisement
Awali, Mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Iringa, Ritha Kabati amesema mikoa hiyo ina vivutio vingi vinavyoweza kuongeza pato la taifa lakini baadhi yake havijulikani.

"Nyanda za juu kusini kuna vivutio vingi sana na tuiombe Serikali iendelee kuwaelimisha wananchi wa mikoa hiyo kutumia vivutio hivyo kujikwamua kiuchumi," amesema Kabati.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz