Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Katavi aagiza madereva wakorofi washughulikiwe

2d95d756470cea4fa3a0e260f9d4b79a RC Katavi aagiza madereva wakorofi washughulikiwe

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: Habari Leo

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame kufuatilia na kuchukua hatua za kisheria kwa madereva wote wanaolalamikiwa kuendesha mwendo kasi katika barabara ya Mpanda - Vikonge.

RC Mrindoko ametoa maagizo hayo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Tanganyika katika mkutano wa hadhara, wakilalamikia madereva hususani gari za abiria pamoja na gari za serikali kuendesha mwendo kasi, bila kujali usalama wa maisha ya wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara hiyo.

Mkazi wa Majalila wilayani Tanganyika, Mnesor Kombakusha akizungumza katika mkutano huo, alisema baadhi ya madereva wanaotumia njia hiyo wamekuwa wakihatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo, kwa kuendesha mwendo kasi, jambo ambalo linaleta hofu ya usalama wa watembea kwa miguu.

Kombakusha amemtaja mmoja wa madereva wanaohatarisha usalama wa wananchi wa Majalila, anayefahamika kwa jina moja la Iddi, ambaye amekuwa akiendesha kwa mwendo kasi katika barabara hiyo.

Pia alisema madereva wa magari ya serikali, wanaotumia njia hiyo, wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani, ambapo wamekuwa wakiendesha mwendo kasi katika maeneo hayo, bila kujali ni maeneo ya makazi.

Chanzo: Habari Leo