Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kagera ataka miti kutengeneza madawati ya watakaojiunga kidato cha kwanza 2019

Thu, 20 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kagera. Mkuu wa Mkoa wa Kagera,  Brigadia Jenerali Marco Gaguti, ameagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuziruhusu halmashauri nane mkoani humo kukata miti kwa ajili ya kutengeneza viti na meza za wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2019.

Ametoa agizo hilo leo Alhamisi Desemba 20, 2018 katika kipindi cha Asubuhi Njema kinachorushwa na Redio Kwizera Wilaya ya Ngara wakati akieleza mkakati wa ujenzi wa vyumba 315 vya madarasa vinavyotakiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu ijayo.

Amesema TFS wakitoa miti,  halmashauri zitatumia mafundi wake na baadhi ya fedha za ruzuku ya Serikali kukamilisha viti na meza badala ya mzigo huo kuachiwa wazazi.

"Mkakati wa Mkoa ni kushirikisha wadau kama taasisi za kibenki na wenye nia njema ya kuunga  mkono juhudi za Serikali kutoa fedha kujenga vyumba vipya vya madarasa kwa kutumia mikutano ya harambee kuondoa changamoto hiyo,” amesema Gaguti.

Wiki iliyopita Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo alibainisha kuwa mikoa ya Kagera na Kigoma ina idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza lakini changamoto ikawa ni vyumba vya madarasa.



Chanzo: mwananchi.co.tz