Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kagera: Hakuna Sukari ya magendo itakayoingia Kagera

RC Kagera , Albert Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila alipotembelea Kiwanda cha Kagera Sugar

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kuhakikisha wawekezaji wa ndani wanalindwa na viwanda vyao, serikali mkoani Kagera imewatahadhalisha wafanyabiashara watakaojihusisha na uingizaji wa Sukari kutoka nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Albert Chalamila January 05, Mwaka huu wakati alipofanya ziara katika kiwanda Cha Sukari Kagera kwa lengo la kujionea uzalishaji kiwandani hapo.

Akiwa kiwandani hapo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapa nafasi wawekezaji wa ndani ambao kwa asilimia kubwa wamekuwa wakichangia katika kukuza uchumi wa Taifa letu.

Chalamila amevutuwa na uwekezaji iliyofanywa katika kiwanda hicho ukiwemo upanuzi wa mashamba ya Miwa lakini na kuwawezesha wakulima wa nje kuuza Miwa yao kiwandani hapo japo kwa asilimia 10% ya Miwa inayochakatwa.

Aidha amesema kuwa kama serikali watakilinda kiwanda hicho ambacho hadi sasa kimezalisha ajira Zaidi ya 10,000 kwa watanzania ambacho pia kimekuwa kikiwajengea uwezo Watanzania kwa kuwasomesha nje ya nchi na baadae kuwaajiri kama wafanyakazi.

Chalamila ametumia fursa hiyo pia kuwaomba wawekezaji wa kilimo kuja Kagera kuwekeza katika kilimo Cha Miwa kwakuwa tayari Soko lipo na Ardhi watapata.

Kwa upande wake mwakilishi wa kiwanda hicho Vincent Mtaka ambaye ni Meneja usafirishaji amesema kuwa lengo lao kama kiwanda ni kuondoa upungufu wa Sukari Nchini ili kuifanya nchi kuacha kuagiza Sukari kutoka nje ya nchi.

Mtaka amesema kuwa ili kuyafikia malengo hayo lazima wawe na mashamba makubwa ambayo wameyaomba kwa serikali.

Ameongeza kuwa katika msimu wa 2021 wamezalisha Tani 120,000 ambapo wanalenga kufikia Mwaka 2025 kuzalisha Tani laki 300,000.

Sambamba na hayo Vincent maeiomba serikali kumalizia kipande Cha Barabara kutoka daraja kitengule hadi Bunazi ili kurahisisha usafirishaji wa Miwa kwenda kiwandani.

Ameongeza kuwa Barabara hiyo pia ni nyenzo Bora ya mawasiliano baina ya wilaya ya Karagwe na Missenyi na itawarahisishia wananchi kufanya shughuli zao za kila siku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live