Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kagaigai akabidhiwa madarasa 44 Rombo

Romboopic Data RC Kagaigai akabidhiwa madarasa 44 Rombo

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai ameupongeza uongozi wa wilaya ya Rombo kwa kuwa wa kwanza kukabidhi ujenzi wa madarasa 44 yaliyotengewa fedha na Serikali Sh880 milioni ambapo amesema kukamilika kwa madarasa hayo kutapunguza changamoto ya msongamano wa wanafunzi darasani.

Akizungumza mara baada ya kukagua madarasa hayo ambayo yamejengwa ndani ya mwezi mmoja na nusu ,RC Kagaigai amesema wanafunzi wote ambao walichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2021 wote watapata nafasi ya kuendelea na masomo.

 “Nimpongeze mkuu wa wilaya hii ya Rombo kwa kazi hii kubwa ambayo ameifanya ya kusimamia na kuhakikisha kazi inafanyika kwa ufanisi mkubwa ,wilaya hii  ndio imekuwa ya kwanza kukamilisha ujenzi wa madarasa haya 44 ambayo yanatokana na fedha ambazo Rais wetu alizipata kwa ajili ya mapambano dhidi  ya uviko 19,”amesema.

Kagaigai amesema Mkoa wa Kilimanjaro ulipata jumla ya Sh5.52 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ili kuhakikisha wanafunzi wote wanakaa madarasani bila msongamano.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga amesema ujenzi huo ulianza Oktoba 26,2021  ambapo mpaka sasa ujenzi  huo wa maradasa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live