Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Kafulila atoa siku 7 Mkataba na Mkandarasi Didia Co. Ltd Uvunjwe

KAFULILAAA Ushirika RC Kafulila

Wed, 18 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila ametoa muda wa siku saba kwa wakala wa Barabara mjini na vijijini (Tarula) Wilaya ya Meatu mkoani humo kuvunja mkataba na Mkandarasi Didia Co.ltd kutoka mkoani Shinyanga ambaye alikuwa anajenga barabara ya Mbaragane – Sulu.

Kafulila amefikia hatua hiyo leo baada ya kufanya ziara wilayani humo na kukagua ujenzi wa Barabara hiyo, na kubaini Mkandarasi huyo ameshindwa kutekeleza makubaliano yaliyomo kwenye mkataba wa ujenzi wa Barabara hiyo.

Katika mkataba huo, Mkandarasi huyo alitakiwa kukamilisha ujenzi wa Barabara hiyo kwa kipindi cha miezi sita, kutoka Novemba 2021 hadi Aprili 2022, ambapo mpaka sasa ameshindwa kukamilisha mradi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live