Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Jokate akemea vikali unyanyasaji wa watoto

18206 Pic+jokate RC Jokate akemea vikali unyanyasaji wa watoto

Wed, 10 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, amekemea vikali sakata la vitendo vya utoro,mimba za utotoni pamoja na suala la ubakaji kwa watoto wadogo vinavyofanywa na baadhi ya watu wazima ambapo ni kinyume na sheria na taratibu za nchi kwani vinachangia kwa kiasi kikubwa kukatisha ndoto zao.

Mwegelo amezungumza hayo wakati akifungua mkutano wa kikao kazi kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na viongozi wa Kata 17 za Wilaya hiyo ambao ni Maofisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Watendaji wa vijiji pamoja na Wenyeviti wa vijiji kwa lengo la kujadili miradi mbalimbali ya maendeleo, huku akiwataka viongozi hao kuacha tabia ya kugombana na badala yake kujadili changamoto zinazowakabili.

Mwegelo amesema lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawaletea wananchi maendeleo ikiwemo kutoa elimu bora, hivyo hawezi kulifumbia macho suala la watoto kutokana na vitendo wanavyofanyiwa na kuwataka wale wote ambao watabainika kuhusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hivyo.

“Mkutano huu ni muhimu sana katika suala zima la kuleta maendeleo kwa wananchi wetu wa Wilaya ya Kisarawe, kwani tumeweza kuwakutanisha maofisa tarafa,watendaji wa kata, watendaji wa vijiji pamoja na wenyeviti mbalimbali wa vijiji, hivyo ninawaomba masuala yote ambayo tutayajadili hapa ni lazima tuyafanyie kazi hasa hii changamoto ya watoto wetu kufanyiwa vitendo vya ubakaji na watu wazima na wengine kujikuta wanakatisha masomo yao ni vema tukashirikiana kuanzia ngazi za chili ili kulitafutia ufumbuzi suala hili,”amesema Jokate.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mussa Gama amesema kwamba lengo la kuwakutanisha viongozi na wawatendaji hao ni kufanya tatmini ya utekelezaji wa majukumu ya kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo katika ngazi husika ambapo pia ameahidi kuvalia njuga maagizo yote ambayo yametolewa na Mkuu wa Wilaya hasa suala la watoto wadogo kubakwa.

Aidha, Gama amesema kuwa katika kikao kazi hicho kimeweza kuweka mipango mikakati kwa viongozi na watendaji katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo, ikiwemo katika masuala ya kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo sambamba na kufanya kazi kwa weledi na kuwatumikia wananchi wao kwa hali na mali lengo ikiwa ni kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo,” amesema Gama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live