Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Iringa amshukia mkandarasi ucheleweshaji ujenzi wa daraja

Daraja Iringa (600 X 328) RC Iringa amshukia mkandarasi ucheleweshaji ujenzi wa daraja

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa iringa Queen Sendiga amesema hayupo tayari kumuongezea muda mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Ujenzi wa daraja la tosamaganga ambalo kwa muda mrefu limekuwa hitaji la wananchi.

Daraja hilo linalojengwa na mkandarasi GS Contractors ya Iringa na kusimamiwa na wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA Wilaya ya Iringa linatakiwa kukamilika ifikapo January 17/2022 kwa Gharama ya zaidi ya shilingi Milioni 600 huku Ujenzi wake ukifikia asilimia 75%

Baada ya kutembelea na kukagua Ujenzi huo Sendiga amemtaka mkandarasi kuongeza kasi kwani anaona dalili za kususua jambo ambalo halikubaliki na kumpa muda hadi ifikapo January 30 mwakani Daraja hilo liwe limekamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live