Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Iringa: Wanawake acheni kutukanana mtandaoni

Ulevi Pic RC Iringa: Wanawake acheni kutukanana mtandaoni

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego amesema nyakati hizi wanawake hawatakiwi kusubiri kusukumwa, bali watafute fursa hata kupitia simu janja walizonazo ambazo zina taarifa zote.

“Wakati mwingine si rahisi kiongozi kumfikia kila mwanamke alipo, ila kwa kutumia simu zetu tuache kutukanana na kukashifiana kwenye mitandao ya kijamii, tuzitumie kujengeana uwezo na kujengeana ujasiri hapo lazima tutatoka,” amesisitiza. Dendego amesema mwanamke ni jeshi kubwa, kwamba hayo yamesemwa hata kwenye vitabu vya dini, hivyo wanatakiwa kuwa chachu ya mabadiliko.

“Sasa hivi kuna ongezeko kubwa la uvunjifu wa maadili na wanawake wamekuwa wakishiriki moja kwa moja, kusherehesha mambo mabaya yanayotokea kwenye mitandao ya kijamii.

“Wanawake turudi nyuma, tukatae kuwa sehemu ya kusherehesha au kufurahia kuona mmomonyoko wa maadili unapotokea au mwanamke mwenzetu anapopata shida, kunyanyaswa mitandaoni tuwe wakemeaji na wafariji wa wanawake wanapopata matatizo,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live