Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Homera asitisha posho za watumishi wote wa halmashauri

Mkuu Wa Mkoa Wa Mbeya Mhe Juma Homera RC Homera

Sat, 23 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesitisha utoaji wa posho kwa watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya Kyela mkoani isipokuwa madiwani na kutaka zikatumike kukamilisha ujenzi wa shule tano za msingi ambazo miradi yake  imeonyesha kusuasua.

Homera ametoa agizo hilo jana Septemba 22, 2023  baada ya kutorishiwa na utekelezaji wa miradi hiyo ambayo ilipokea fedha kutoka Serikali hali iliyosababisha  kuchukua hatua za kuwasimamisha kazi watumishi wanane wakiwemo walimu wakuu watano, wahandisi wawili na ofisa manunuzi.

“Ile asilimia 40 inayokwenda kwenye maendeleo na ile nyingine 60 za posho kuanzia sasa hazitatolewa kwa watumishi na badala yake zitaelekezwa kukamilisha ujenzi wa miradi ya elimu isipokuwa madiwani pekee walipwe posho zao,”amesema.

Amesema katika asilimia hizo zinazotolewa na halmashauri kwa sasa watakaopata ni madiwani pekee lakini kwa upande wa watumishi zimesitishwa mpaka hapo miradi ya elimu itakapokamilika na wanafunzi kuanza kupata huduma.

Aidha ameagiza watumishi wote ambao wako kwenye kamati za ujenzi kutokusafiri kwenda nje ya mkoa mpaka hapo miradi hiyo itakapo kamilika katika Shule za Kasumuru, Mapinduzi, Luteba, Uhuru na Mababu Wilaya ya Kyela.

“Ndugu zangu tumuonee huruma huyu mama Rais Samia Suluhu Hassan anapotafuta pesa na kuleta lengo lake kuleta maendeleo kwa wananchi na kuboresha sekta ya elimu sasa inapofika halmashauri zote zikamilishe miradi mwezi June nyie mpaka sasa haijakamilika,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live