Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera amepiga marufuku ujenzi wa sakafu ya saruji katika miradi mbalimbali ikiwemo madarasa na mabweni ya wanafunzi katika Wilaya ya Rungwe Mkoani humo.
Homera ametoa katazo hilo akiwa katika ziara ya siku tatu Wilayani Rungwe, ambapo ametembelea na kukagua ujenzi wa mabweni katika shule ya tukuyu sekondari na kukuta sakafu ya saruji ambayo ni kinyume na muongozo wa ujenzi kwa Mradi huo unaihitaji kujengwa kwa marumaru au sakafu ya tarazo.
Mbali na katazo hilo Homera ametoa siku 20 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, kuhakikisha wanaondoka sakafu hiyo ya saruji iliyojengwa katika bweni hilo na kuweka marumaru kama muongozo unavyo hitaji.