Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Homera aagiza RITA kutoa elimu ya wosia kwa wanandoa

Mbeya Pic RC Homera aagiza RITA kutoa elimu ya wosia kwa wanandoa

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ameagiza Wakala ya Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) kuhakikisha wanawafikia wananchi wengi hasa wa vijiji na kuwapa elimu ya kuandika wosia wa mirathi ili kupunguza migogoro ya kifamilia kwa wajane au wagane.

RC Homera amesema hayo Novemba 9, kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria na kufanyika kitaifa mkoani Mbeya katika uwanja wa Ruanda Nzovwe.

"Tunaomba mwafikie wananchi na kuwapatia elimu ya kuandika wosia wa mirathi kwa wanandoa, kwani tunapokea kesi za malalamiko ya wanawake kuporwa mali wanapofiwa na waume zao," amesema.

Homera ameongeza kuwa mira na desturi pia ni changamoto hivyo wakipata elimu ya kutosha itasaidia serikali kutopokea migogoro ya umiliki wa mali katika ngazi za familia ambazo kwa kiasi kikubwa uchumwa na wanandoa.

Ofisa Msajili Msaidizi, Joseph Mwakatobe amesema kuwa wamepokea ushauri huo na kwamba wamejikita zaidi kuwafikia wananchi wengi.

"Agizo hilo ni miongoni mwa majukumu yetu na kupitia maadhisho haya ambayo kilele ni Novemba 12 mwaka huu, tutakuwa tumewafia wananchi wengi zaidi wa rika tofauti wakiwepo walio ndani ya ndoa," amesema.

Naye mkazi wa Ilomba jijini Mbeya, Tausi Mwakyusa ameomba Rita kuwafikia kuwapatia elimu kuanzia ngazi za mashina mitaa na vijijini kuwapata ambayo itashawishi waume zao kuandika wosia wa miradhi na kuwaondoa kwenye manyanyaso pindi wenza wao wanapotangilia mbele za haki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live