Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Hapi awapa onyo Madiwani Rorya

Happypic Hapi awaonya madiwani wanaotaka kuvunja sheria ya ununuzi Rorya

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi amewataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya kumuacha mkuu wa wilaya hiyo, Juma Chikoka (Mchopanga) asimamie utekelezaji wa malekezo ya Ofisi ya Rais (Tamisemi) kuhusu fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa.

Hapi ametoa agizo hilo baada ya kuwepo kwa taarifa za baadhi ya madiwani kutaka kupewa tenda za usambazaji wa baadhi ya vifaa katika kata na vijiji miradi hiyo inapotekelezwa hali aliyosema kuwa haikubaliki.

Akizungumza kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa ya sekondari katika baadhi ya kata wilayani Rorya, RC Hapi amesema kuwa miongoni mwa maelekezo yaliyotolewa na Tamisemi wakati wa utekelezajai wa miradi hiyo ni pamoja na ununuzi wa pamoja wa vifaa vitakavyotumika katika ujenzi wa miradi hiyo.

"Sisi tumeelekezwa kufanya 'bulk procurement' (ununuzi wa pamoja) kwenye ununuzi wa vifaa vya ujenzi lakini hapa kuna viongozi wa kisiasa wakiwepo madiwani wanataka wapewe tenda wao hili jambo haliwezekani lazima tusimamie utaratibu tuliopewa," amesema Hapi.

Akitoa mfano mradi wa ujenzi wa madarasa manne katika shule ya sekondari Nyathorogo iliyo katika hatua ya msingi, amewataka madiwani wenye hoja tofauti juu ya utaratibu wa ununuzi kuziwasilisha Tamisemi.

"Mwacheni Mkuu wa Wilaya asimamie maelekezo tuliyopewa na bahati nzuri nyie wana Rorya mna mkuu wa wilaya mchapakazi.

“Hapa tunachofanya tunasimamia maelekezo ya bosi wetu na kama mna hoja wasilisheni Tamisemi endapo tutaagizwa vinginevyo tutafanya ila kwasasa tunasimamiama maelekezo yaliyotolewa awali na kama mjuavyo Mara tumejiwekea malengo ya kukamilisha miradi hii ifikapo Disemba Mosi Mwaka huu," amesema Hapi.

Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Rorya, Juma Chikoka amesema kuwa licha ya changamoto hizo, wilaya yake inajitahidi kutekeleza miradi hiyo kwa kasi na ubora.

Amesema kuwa wilaya yake imepokea zaidi ya Sh2.34 bilioni kwaajili ya ujenzi wa madarasa 113 ambapo madarasa 98 ni ya shule za sekondadi pamoja na bweni moja

Kuhusu miradi iliyochelewa kuanza, DC Chikoka amesema kuwa ofisi yake itaongeza kasi ya usimamizi ili miradi hiyo iweze kukamilika katika muda uliopangwa na mkoa.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nyaburongo, Marwa Sama amesema kuwa wapo tayari kufauta maelekezo ya serikali ili kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo kwa wakati.

"Tumemsikia RC hayo yote yatarekebishwa na tutatoa ushirikiano ili miradi ikamilike hatuko tayari kukwamisha miradi au kwenda kinyume na serikali," amesema Diwani Sama.

Chanzo: mwananchidigital