Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Hapi atoa wiki mbili wakurugenzi kutafuta Tsh.Bilioni 1.7

Hapi Ali Ziara ya Rais Samia Mkoani Mara iliibua madudu kadhaa ya ubadhirifu

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi ametoa wiki mbili kwa wakurugenzi wa halmashauri tisa zilizopo mkoani humo kuhakikisha jumla ya shilingi bilioni 1.7 za mapato ya ndani ambazo hazijaingizwa benki ziwe zimeingizwa.

Aidha Hapi amewataka wakuu wa wilaya kuchunguza utolewaji mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya wanawake, watu wenye ulemavu na vijana na kuongeza kuwa ndani ya muda huo iwapo wahusika waliokula fedha hizo watabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani humo, Samweli Kiboye naye amewaagiza wenyeviti wa halmashauri za Mkoa wa Mara kuhoji juu ya madai ya upotevu wa fedha hizo kwa wakurugenzi wao.

Hayo yanakuja kufuatia maagizo aliyoyatoa Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake mkoani humo ambapo alimuagiza mkuu huyo wa Mkoa wa Mara kuchukua hatua kwa baadhi ya watendaji ambao wanatuhumiwa katika upotevu huo wa fedha za miradi ya maendeleo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live