Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Hapi ashangazwa na taarifa za kulazwa makaburini

33858 Pic+hapi Tanzania Web Photo

Fri, 28 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amewahoji viongozi wa dini na wazee wa kimila mkoani humo inawezekanaje yeye kulazwa makaburini na wao wapo.

Hapi ameuliza swali hilo katika kikao cha tathimini ya huduma ya matibabu kwa wazee mkoani humo na kusema hayupo atakayeweza sio tu kumlaza makaburini bali hata nje ya kibaraza cha  nyumba yake.

Amesema  wazee wa dini kila siku wanawaombea viongozi wao hivyo hizo ni propaganda za watu walioshindwa na kukosa ajenda.

Amewataka  wananchi wa Iringa wazipuuze taarifa hizo kwani hakuna kitu kama hicho na hakitatokea.

 “Wakati nakuja Iringa nimepiga hodi kwa wazee wa kimila na viongozi wa dini, hivi mzee Malangalila mie naweza kulazwa makaburini na wewe upo? Sheikh wa mkoa na maaskofu kweli?.”

“Huko mtandaoni kuna mtu amezusha kuwa nililala makaburini, bahati nzuri tukawajua ni watu wa upande wa pili,” amesema na kuongeza:

“Wakuu wote wa mikoa tulikuwa kwenye vikao Dodoma na Rais John Magufuli cha ajabu akaibuka mtu mmoja akasema nimelala nimeamka nikajikuta nipo kwenye makaburi ya wapi sijui hata hajayasema. Nitumie fursa hii kuwatoa wasiwasi wananchi wa Iringa wazee hawa viongozi wa dini na wazee wa kimila wako imara kwelikweli na mimi mwenyewe nipo imara kwelikweli kwa sababu tunamcha Mungu.”

“Kama walijua wamenipa hofu basi wameniimarisha zaidi, kwa hiyo nipo imara zaidi na kadri wanavyoleta mashambulizi ndiyo wanazidi kuniimarisha, mimi nitaendelea kuwatumikia wananchi wa Iringa hiyo mishale midogo midogo haiwezi kunivunja moyo,” amesema.

Hapi amesema alichokiona kwa mtu aliyeeneza taarifa hizo aliyemtaja kwa jina la Hilda Newton kuwa kitu pekee cha kukifanyia kazi ni tabia yake ya kutukana watu na kueleza maneno ya kejeli na kufedhehesha viongozi tabia inayohitaji kushughulikiwa.

“Tunayo sheria ya mitandao vyombo vya dola vitashughulika nae na jamii pia imsaidie kubadili tabia ya kutukana na kuwa raia mwema, mimi binafsi natamani nimuone tu nimsamehe maana hajui alitendalo,” amesema.

Soma zaidi: Kauli ya RC Hapi kuhusu Hilda wa Chadema yamuibua Zitto, Mchungaji Msigwa

 

Kwa upande wake, Chifu wa Wahehe mkoa wa Iringa, Gerlad Malangalila amesema mchawi peke yake ni shule, Ally Hapi babake na mamake ndio waliomloga kwa kumpa elimu.

“Mmenitia aibu kutoa katika mitandao eti Ally Hapi amekutwa kwenye makaburi amevaa bukta yamenikuta nikiwa ni kiongozi wa mila na desturi yameniuma sana na kunisikitisha,” amesema.

Amesema watu wa Iringa waone aibu kutamka vitisho kwa watoto wa watu visivyokuwa na maana ili washindwe kuongoza kwa ajili ya maneno yao.

“Hapi alipoingia Iringa uongozi wa mkoa ulituita kitu tulichomfanyia mkuu wa mkoa habari zote zilitapakaa kwenye mitandao nikaanza kuulizwa kwa nini umemsimika  u chifu Ally Hapi, je ni kweli nilimsimika u chifu Hapi aliwauliza wazee wa kimila waliokuwamo ndani ya ukumbi huo.

Soma zaidi: Hilda wa Chadema amgomea RC Hapi

 

“Mgeni unapomkaribisha ndani kwako huwa hawampi kiti? je huwezi kumpa vazi lako la jadi akavaa?  nilichofanya cha ajabu ni nini mpaka nitukanwe kwenye mitandao,” Alihoji.

Soma zaidi: RC Hapi aagiza polisi kumkamata Hilda wa Chadema popote alipo

 

Soma zaidi: Bavicha watia mguu sakata la RC Hapi, Hilda wa Chadema

 



Chanzo: mwananchi.co.tz