Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Hapi aipa hospitali ya rufaa Iringa siku 30 kujirekebisha

12248 HAPI+PIC TanzaniaWeb

Thu, 16 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ametoa siku 30 kwa uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Iringa kujitathimini kama wana uwezo wa kuendelea kuwahudumia wananchi wanaofika kupata huduma.

Hapi ametoa agizo hilo leo Agosti 16 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo na kusema kuwa amepokea malalamiko mengi juu ya huduma mbovu inayotolewa katika hospitali hiyo hasa kauli mbovu zinazotolewa na wauguzi.

Pamoja na lugha chafu, pia Hapi amesema amepokea malalamiko ya upotezaji wa mafaili ya wagonjwa na baadhi ya madaktari kufika hospitalini  wakiwa wamelewa na kukithiri kwa vitendo rushwa kwa watoa huduma.

“Dawa hakuna wakati serikali inatenga fedha nyingi kwa ajili ya dawa, pia baadhi ya huduma huchelewa kufunguliwa na kuwahi kufungwa hali ambayo haitavumilika katika kipindi changu cha uongozi” amesema Hapi

Amesema ameamua kutembelea hospitali hiyo kwa kushtukiza ili kujua tatizo liko wapi na kwa nini wananchi hawahudumiwi vizuri.

Hivyo akatoa maagizo katika uongozi wa hospitali na watendaji wake kujitathimini.

 “Naagiza uongozi wa hospitali kujitathimini ndani ya kipindi kifupi kisichozidi mwezi mmoja, wajitathimini jinsi wanavyotoa huduma kwa wananchi wetu sitaki kusikia mafaili ya wagonjwa yanapotea wala wanatukanwa na kujibiwa lugha chafu,”amesema Hapi.

 Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi Charles Lema ambaye pia ni Daktari Bingwa wa mifupa amesema wameyapokea maagizo ya Mkuu wa Mkoa na kuyafanyia kazi kadri iwezekanavyo.

“Baadhi ya malalamiko tunayajua na tulikuwa tunayafanyia kazi, suala la upotevu wa mafaili tulikuwa tunalijua lakini suala la kutoa rushwa hatuna taarifa nalo na tumekuwa tukilifanyia kazi, suala la lugha tulikuwa tunalifahamu na tumekuwa tukilifanyia kazi kila siku,”amesema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz