Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Hapi adai yupo tayari kutumwa popote na Rais Samia

HAPI WEBBB Ed RC Hapi adai yupo tayari kutumwa popote na Rais Samia

Tue, 15 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Hapi ametoa kauli hiyo hii leo Juni 15, 2021, jijini Mwanza, wakati akizungumza kwenye mkutano wa Rais Samia na vijana ambapo amemuahidi kuwa wao kama vijana wataendelea kumpa ushirikiano na kwamba yupo tayari kutumwa popote pale.

"Mheshimiwa Rais kwa niaba ya vijana wote ambao umekwishatuteua kwenye serikali yako, tungependa kukushukuru sana kwa imani yako kubwa kwa vijana, nchi yetu wakati inapata uhuru Baba wa Taifa alikuwa na miaka 39 na Mzee Kawawa alikuwa na miaka 35 leo unazungumza na kundi lililoshiriki katika nchi yetu kuhakikisha tunapata ukombozi,"

"Vijana sisi tutakuunga mkono, tutakutii, tutapokea maelekezo yako, tutafanya kazi usiku na mchana popote pale utakapotupeleka kuhakikisha dhamira yako kwa vijana na kwa Tanzania inaenda kutimia, unalo jeshi la vijana nyuma yako ambao wako tayari kukusaidia kuitekeleza Ilani ya CCM". amesema RC Hapi.

Chanzo: ippmedia.com