Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Gambo ataka polisi kudhibiti uhalifu mipakani

88501 Gambo+pic RC Gambo ataka polisi kudhibiti uhalifu mipakani

Sat, 14 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha,  Mrisho Gambo amewataka makamanda wa polisi Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kushirikiana kudhibiti uhalifu kwenye mipaka kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka 2019.

Ametoa agizo hilo leo Jumamosi Desemba 14, 2019 wakati katika mkutano wa makamanda wa polisi Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kuandaa mikakati na mbinu shirikishi za kupambana na  uhalifu.

Gambo amesema kumekuwa na  matukio ya uhalifu mwishoni mwa mwaka,  ni muhimu kushirikiana kuyathibiti.

Mkurugenzi wa Intelejensia wa polisi, Charles Mkumbo amesema  ni muhimu kuongeza mshikamano kwa makamanda hao ili kukomesha uhalifu.

Kamishna  msaidizi mwandamizi wa polisi,  Edward Bukombe amesema wakati wananchi wakijiandaa kusherekea sikukuu wahalifu  nao hujipanga kufanya uhalifu, “tumejipanga kukomesha vitendo hivyo  kwa kuimarisha ulinzi kwenye mipaka.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz