Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Gambo agiza kusimamishwa kazi maofisa wawili Karatu

73609 Gambo+pic

Fri, 30 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Karatu. Mkuu wa Mkoa Arusha (RC) nchini Tanzania, Mrisho Gambo ameagiza kusimamishwa kazi ofisa manunuzi wa halmashauri ya Karatu Modestus Kastila na Kaimu Mhandisi wa ujenzi wa Wilaya, Venance Malamla kwa kushindwa kusimamia mradi wa soko la Karatu na hospitali ya wilaya.

Gambo ametoa agizo hilo leo Ijumaa, Agosti 30, 2019 baada ya kutembelea soko kuu la Karatu na kupokea kero za wafanyabiashara wa soko hilo.

Mkuu huyo wa mkoa pia ametangaza kuunda kamati maalum ya uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za mradi wa soko hilo na kushindwa kufuatwa taratibu za manunuzi.

"Kutokana na kushindwa kusimamia ujenzi wa soko la Karatu na wewe ofisa manunuzi kuruhusu fedha kutoka ile hali vifaa vya ujenzi vikiwa havijafika eneo husika nawasimamisha kazi kupisha uchunguzi," amesema

Amesema  Kaimu mhandisi wa ujenzi halmashauri, Malamla  ameshindwa kumudu majukumu yake ipasavyo ikiwemo kushindwa kutoa ramani sahihi ya ujenzi wa soko, pamoja kushindwa kukadiria malighafi za ujenzi wa hospitali ya wilaya.

Awali, wafanyabiashara wa soko hilo, walieleza tangu kuvunjwa soko la zamani wamekuwa wakifanya biashara katika mazingira magumu ikiwepo kukosa ulinzi na taka kushindwa kuzolewa.

Pia Soma

Advertisement   ?
Hata hivyo, mkurugenzi wa halmashauri Karatu, Moris Waziri amesema halmashauri hiyo, itawalipa malimbikizo ya nyuma ya madeni walinzi na akawataka wafanyabiashara kuchangia usafi wa soko na ulinzi.

Waziri pia aliagiza wafanyabiashara wote kuwa na vitambulisho vya machinga kama wanataka kuendelea kufanya biashara katika soko hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz