Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Gabriel atoa siku 7 kwa waliopoteza mapato

Rcmwanza2 RC Gabriel atoa siku 7 kwa waliopoteza mapato

Thu, 17 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel ametoa siku saba kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa mkoa huo kuwasilisha kwenye vyombo vya dola majina ya wakusanya mapato ya Halmashauri ya Sengerema waliohusika na upotevu wa zaidi ya shilingi milioni 350 ili wachukuliwe hatua.

Submitted by Elbogast on Alhamisi , 17th Jun , 2021 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi RC Robert Gabriel

Mhandisi Robert Gabriel ametoa kauli hiyo kwenye kikao maalum cha kujadili utekelezaji wa hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Halmashauri hiyo kwa kipindi cha kuishia Juni 30, mwaka 2020 ambapo kwa kipindi hicho Halmashauri ya Sengerema ilipata hati yenye mashaka hali iliyomlazimu kutoa agizo la kukamatwa kwa wakusanya mapato hao.

"Ndani ya wiki moja tunataka tupate majina ya hao watu waitwe, tukimaliza hiki kikao barua ziandikwe leo hii msiondoke ofisini, watu waitwe na wote watafutwe, kitengo cha fedha kikaguliwe ili tuone kwa namna gani kitoe taarifa za mapato, kwani hata tunayopata ni madogo," amesema RC Gabriel.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema Yanga Makaga akaahidi kutoa ushirikiano katika kuwabaini waliohusika na upotevu wa fedha hizo kwani wengi wao ni watumishi wa umma na majina yao tayari yapo.

Aidha, Katika hatua nyingine RC Gabriel amezihimiza Halmashauri kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato kwani vyanzo vya mapato vipo.  

Chanzo: eatv.tv