Wed, 20 Sep 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mafuta yapo ya kutosha katika mkoa huo.
Chalamila amelazimika kutoa ufafanuzi huo mbele ya Waziri Mkuu na Naibu waziri Mkuu katika Kongamano la Nishati ambalo linafanyika Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Chalamila, kuna minong'ono inayosambaa kuhusu kukosekana kwa Nishati hiyo jijini humo na amewataka watumiaji wa nishati hiyo kupuuza taarifa hizo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live