Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Chalamila kazikazi, apokea Mwenge wa Uhuru

RC Chalamila Kazikazi, Apokea Mwenge Wa Uhuru RC Chalamila kazikazi, apokea Mwenge wa Uhuru

Wed, 24 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Mei 24,2023 amepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoa wa Pwani katika viwanja vya Tazara -Temeke Jijini Dar es Salaam.

Akiongea wakati wa mapokezi ya Mwenge huo RC Chalamila amesema Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Dar es Salaam utakimbizwa katika umbali wa KM 499.9 kwa kupitia miradi 32 yenye thamani ya Shilingi Bilioni Tisini na Tatu, Milioni Mianne Hamsini na Saba Laki Nne na Elfu sitini na Saba, Mia Tatu Sitini na Nane na Senti Themanini na Tatu (93,457,467,363,.83)

Aidha RC Chalamila amesema miradi hiyo ipo iliyokamilika na mingine ipo katika hatua mbalimbali za Utekelezaji

Mhe Albert Chalamila amekabidhi mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya Temeke ambayo ndiyo Wilaya ya Kwanza kukimbiza Mwenge huo katika Mkoa huo, ambapo Tarehe 25/05/2023 utakabidhiwa Wilaya ya Kigamboni, Tarehe 26/05/2023 Wilaya ya Ilala, Tarehe 27/05/203 Wilaya ya Ubungo na Tarehe 28/05/2023 Wilaya ya Kinondoni na baadae utakabidhiwa Mkoa wa Kusini Magharibi - Zanzibar.

Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 unachagizwa na kauli mbiu ya " Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa "

Chanzo: www.tanzaniaweb.live