Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Chalamila atumia spika ya Mchungaji Mashimo kuhutubia wananchi

Chalamila Mashimo Mbezi.png RC Chalamila atumia spika ya Mchungaji Mashimo kuhutubia wananchi

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchungaji Daud Mashimo amejikuta akigeuka lulu katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kituo cha daladala Mbezi Mwisho baada ya vifaa vyake vya kuhubiria kutumiwa kuhutubia wananchi.

Chalamila ametembelea kituoni hapo leo Oktoba 12, 2023 kujionea hali ya utoaji wa huduma ya usafiri wa magari yaendayo haraka ambapo pia alizungumza na wananchi.

Mashimo ambaye amekuwa akitumia kituo hicho muda mrefu kuhubiri neno la Mungu, aligeuka lulu baada ya vifaa vyake anavyotumia kuhubiri ikiwemo spika na kipaza sauti kutumiwa na Mkuu wa Mkoa.

Baada ya kufikia eneo hilo Chalamila alizunguka katika sehemu kadhaa za wafanyabiashara kisha akauliza 'Mashimo uko wapi?,' na yeye kujitokeza haraka kuweka spika na kumpa kipaza sauti ili aweze kuzungumza na wananchi waliokuwa eneo hilo.

Mashimo aliyekuwa amevalia suti nyeusi, alionekana kubeba spika hiyo na kuongozana na msafara wa mkuu huyo wa mkoa kila ulipopita.

Mashimo amesema anajisikia faraja kutoa huduma hiyo kwa kuwa ni jambo la kuwaletea maendeleo wananchi.

Katika hatua nyingine Mashimo aliwachongea baadhi ya watu wanaotumia maeneo ya Serikali yakiwemo ya wazi kuwauzia wafanyabiashara wadogo maarufu 'Wamachinga'.

Amesema wapo wanaouziwa maeneo hayo hadi Sh700,000 na kutaka uongozi wa mkoa kuwashughulikia kwani baadhi yao wapo watendaji wa Serikali na watu binafsi.

Akijibu hilo, Chalamila amesema analijua na kueleza wameanza kushughulilia suala hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live