Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Chalamila akemea rushwa mabaraza ya ardhi

RC Chalamila Akemea Rushwa Mabaraza Ya Ardhi RC Chalamila akemea rushwa mabaraza ya ardhi

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: Eatv

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila amewataka wajumbe wa baraza la ardhi katika mkoa huo, kuacha vitendo vya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wananchi, maana kufanya hivyo kunachochea migogoro ambayo athari zake ni kubwa ikiwamo watu kuuana

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa kauli hiyo wakati wa kuwaapisha wajumbe wa baraza la ardhi kutoka katika wilaya ya Kyerwa, na kuwataka kutofanya kazi kwa kuingiliwa na mtu au chombo chochote katika maamuzi yao, ili waweze kutenda haki

"Wengi mnaapa hapa lakini mnakwenda kukengeuka na mnawanyanyasa na kuwaonea watu, na mwisho inakuja kuonekana kwamba baraza la ardhi ni mdudu ambaye anawanyang'anya haki Watanzania," amesema Chalamila.

Nao wajumbe wa baraza la ardhi wilaya ya Kyerwa walioapishwa, wameahidi kutenda haki na kwa haraka, ili kuwaondolea wananchi tatizo la kuacha shughuli zao kila mara kwenda kufuatilia kesi.

"Kule kuzungushwa mara nenda rudi kesho hiyo wasitarajie kwamba itakuwepo, na tutahakikisha hakuna kudai malipo kutoka kwa mtu yeyote anayetafuta haki, lakini pia tutakusanya maoni kutoka kwa wananchi tujue wanasema nini kuhusu utendaji kazi wetu, tufanye nini na wapi mambo yamepindishwa," wamesema.

Wilaya ya Kyerwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2013 haijawahi kuwa na baraza la ardhi, hali ambayo imekuwa ikisababisha wananchi kusafiri umbali mrefu kwenda kufuata huduma hiyo katika wilaya jirani ya Karagwe.

Chanzo: Eatv