Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Chalamila akemea biashara ya magendo

Chalamila Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila

Sat, 20 Aug 2022 Chanzo: eatv.tv

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila amesema pamoja na wilaya ya Kyerwa kuzalisha kwa wingi zao la kahawa, bado ipo nyuma kimaendeleo kutokana na usaliti unaofanywa na baadhi ya wananchi, viongozi na watumishi wa serikali, kwa kuhusika na biashara ya magendo ya Kahawa kwenda nje ya nchi

Akizungumza na wananchi, viongozi na watumishi wa serikali wakati wa ziara yake aliyoifanya katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kyerwa ikiwamo ya Murongo na Nkwenda, Chalamila amesema kuwa anawafahamu hata kwa majina viongozi wa Halmashauri, wa chama, Askari, mgambo na hata wananchi ambao wanahusika katika usaliti huo, na kwamba atakabidhi orodha hiyo kwa mamlaka zinazohusika ili uchunguzi uanze mara moja.

Amesema serikali ya mkoa haiwezi kuendelea kumuomba fedha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuboresha huduma ikiwamo barabara, wakati wanaruhusu Kahawa zitoke kwa magendo

Chanzo: eatv.tv