Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Chalamila agiza taasisi za serikali ikiwamo majeshi zikatiwe maji

86212 Pic+chalamila RC Chalamila agiza taasisi za serikali ikiwamo majeshi zikatiwe maji

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (RC) nchini Tanzania, Albert Chalamila ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mkoani Mbeya (Mbeya- WSSA) kuzikatia maji taasisi zote za serikali endapo hazitalipa madeni ya maji wanazodaiwa ifikapo Desemba 15, 2019.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu huyo wa mkoa leo Jumatano Novemba 27, 2019 katika kikao cha Kamati Ushauri ya Mkoa huo kilichofanyika jijini Mbeya.

Chalamila amesema endapo mkurugenzi wa idara hiyo hatochukua hatua hiyo atahakikisha anasimamia kuhakikisha anaondolewa kwenye nafasi hiyo.

"Kata maji kote na baada ya hapo tutazungumza Kiswahili kinachofanana, maana itaonekana Mbeya kama hatukusanyi mapato kumbe madeni yako kwa watu," amesema.

 Chalamila amemtaka Mkurugenzi kuwasilisha ofisini kwake maelezo ya wadaiwa ili awaandikie barua huku nakala nyingine ya barua akiahidi kuipeleka kwa Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Awali, akizungumza Mkurugenzi wa Mbeya- WSSA, Ndele Mengo amesema idara hiyo inadai jumla ya Sh4.6 Bilioni huku Sh1.85 bilioni ikizidai taasisi za serikali.

Miongoni mwa taasisi hizo ni Jeshi la Polisi linalodaiwa Sh666 milioni, Magereza Sh231 milioni, Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ) Sh50 milioni, Mbeya Jiji Sh109 milioni na Idara ya Afya Sh45 milioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz