Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Chalamila abomoa nyumba ya mkazi wa Mbeya

115243a5795d6af7102d60b239417171 RC Chalamila abomoa nyumba ya mkazi wa Mbeya

Thu, 17 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesimamia operesheni ya kubomoa nyumba ya Athony Lyuba mkazi wa mkoa huo iliyopo Kata ya Inyala, baada ya kukaidi agizo la kubomoa kwa hiyari nyumba yake.

“Nimeamua nibomoe mwenyewe nyumba yako maana mara nyingi tulikuomba ufanye jambo hili kwa hiyari lakini ulileta ukaidi, haiwezekani wengine wote wakubali kutekeleza agizo la ubomoaji lakini wewe peke yako ugome kama ni imani za kishirikina basi tutaziona” amesema Chalamila.

Uamuzi wa Chalamila ulitokana na mtu huyo kukaidi agizo lililowataka wakazi wa eneo hilo kubomoa nyumba zao ili kupisha mradi wa ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 16.7 kutoka Inyala hadi Simambwe.

Chanzo: habarileo.co.tz