Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Chalamila aagiza mawakala mashine za EFD kukamatwa

86560 RC+pic RC Chalamila aagiza mawakala mashine za EFD kukamatwa

Sun, 1 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya nchini Tanzania, Albert Chalamila ameagiza mawakala wa mashine za kutoa risiti za kielektroniki (EFD)  kukamatwa na kuwekwa ndani kutokana na kutohudhuria mkutano wa wafanyabiashara soko la Sido, jijini Mbeya.

Chalamila ametoa agizo hilo leo Jumamosi Novemba 30, 2019 katika mkutano wake na wafanyabiashara wa soko hilo kwa ajili ya kusikiliza kero zao.

"RPC (kamanda wa polisi Mkoa) watafute leo Jumamosi wapumzike mahali tutakutana nao Jumatatu, haiwezekani huu ni upuuzi tunawahitaji wao hawapo hata sisi tumeacha usingizi," amesema.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoani Mbeya (TRA),  Jiji la Mbeya lina mawakala wanne kwa sasa ambao walitakiwa kuhudhuria mkutano huo.

Chanzo: mwananchi.co.tz