Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Chalamila: Suala la ajali ya ndege ni mtambuka

Operanews1667739281273 Chalamila RC Chalamila

Mon, 14 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila, amesema Kampuni ya ATR ya Ufaransa iliyotengeneza ndege yenye namba ATR 42-5H PWF mali ya Shirika la Precision Air, iliyopata ajali Novemba 06, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 19, wamefika mkoani humo na kufungua vifaa vinavyohitajika kwa uchunguzi.

Chalamila ameyasema hayo, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu vipaumbele vya Mkoa wa Kagera, anavyotarajia kuvitekeleza akiwa mkoani humo.

“Suala la ajali ya ndege, naweza kusema ni mtambuka, limekaribisha watu wengi, liko chini ya wataalamu wake, serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi, inaendelea na kazi kuhusiana na jambo hilo, kufahamu nini kimesababisha ajali hiyo na nini kinaweza kuja kufanyika baada ya matokeo ya uchunguzi wa ajali hiyo," amesema Chalamila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live