Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Chalamila: Atakayejifanya takataka Januari 24, atasombwa

Chalamila: Changamkieni Fursa Mkutano Wakuu Wa Nchi Afrika RC Chalamila: Atakayejifanya takataka Januari 24, atasombwa

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kuwa mtu yeyote atakayejifanya takataka tarehe 24 Januari 2024, watasombwa kama takataka zingine.

Chalamila amesema hayo kufuatia tamko la Chadema kutangaza maandamano nchi nzima mnamo Janauri 24, 2024 kuishinikiza Serikali kuondoa miswada ya mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa ili kuwapa nafasi wadau kutoa maoni yao.

Hata hivyo Chalamila ametangaza kuwa Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) watakuwa wakifanya usafi jijini Dar mnamo Januari 23-24, 2024 kwa ajili ya kuweka mazingira salama na kuepukana na maradhi ya kipindupindu ambayo yamesambaa katika baadhi ya mikoa nchini.

"Kuna watu wana zagaa zagaa kwenye Tanzanite Bridge, kamateni watu wote wanaokaa kwenye maeneo na walemavu kuombaomba, tumegundua ule ni mtaji wa watu ambao jioni wanakusanya mapato wanawapa kidogo wale walemavu.

"Kwa hiyo walemavu wote wanaombaomba waondolewe mabarabarani kwani Rais ametoa hela kwa ajili ya nyumba za walemavu kwahiyo watakaoendelea kuwepo wakamatwe.

"Asiyetoa mchango au ada ya takataka akamatwe, na ndio maana tarehe 23 na 24 tutafanya usafi kabambe na magari yatakuwepo kubeba taka sasa atakaejifanya takataka na yeye atabebwa.

"Tarehe 20 na 21 nitagawa vifaa vya usafi kwa vyombo vya dola watu wapige kazi mpaka jioni, watu wanachanganya sijui kuna maandano ila sisi tunaendelea na kazi hizo taarifa za maandamano zinapatikana kwa Muliro.

"Huu ugonjwa tunaouzungumzia hapa, ugonjwa ukilipuka mahali ni kiashiria cha vita, maana yake taifa linaweza kuvamiwa, kumekuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani mfano vingunguti.

"Kule Vingunguti Juzi nimeona vijana wanabishana kati ya watu waliopigwa risasi kuwa ni watu wema, walikuwa vijana zaidi ya saba wana mapanga, askari anawazuia wao wanatoa panga kuwapiga hapo kuna haja ya kupigiwa simu mkuu mkoa hapa tufanyaje.

"Na ahidi nitawasafisha wote watakaovunja sheria hilo haliwezi kukubalika, siku tatu hizi natuma vikosi vikasafishe na vijana wote wanaodhani watavunja sheria tunawasafisha," amesema Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live