Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Arusha ataka wazee wapewe matibabu

Fa78fdd7f69569e7333d5547cb5e0892 RC Arusha ataka wazee wapewe matibabu

Wed, 22 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta amemtaka Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha, Dk Kheri Kagya, kuweka mazingira rafiki kwa wazee kupata matibabu katika vituo vya afya.

Alitoa maagizo hayo alipozungumza na viongozi wa Baraza la Wazee wa Arusha jana.

“Wazee hawatakiwi kuhangaika kupata huduma hasa za matibabu, bali watumishi wanapaswa kuwahudumia kwa haraka zaidi,” alisema.

Alisema wazee ni hazina katika ujenzi wa maendeleo ya mkoa kwa kutoa ushauri mbalimbali kadiri ya uzoefu walionao.

Mwenyekiti wa baraza hilo, Mhina Sezua alisema wamefurahi kukutana na mkuu huyo na kuahidi kutoa ushirikiano katika uongozi wake.

Aidha alisema kazi kubwa ya wazee ni kushauri tu pale wanapoona inahitajika kufanya hivyo ili kuleta maendeleo ya mkoa huo kwa ujumla.

Awali akishukuru kwa niaba ya wazee hao, Fauster Licky alisema wazee wamefurahishwa kukutana nao na kusikiliza changamoto zao.

Alisema hiyo inaonesha vipi uongozi wa mkoa unavyowathamini wazee na kuwachukulia kama ni moja ya nguzo za maendeleo ya mkoa huo.

Chanzo: habarileo.co.tz