Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RC Arusha aagiza kusakwa waliofanya vurugu mkutano wa DC Monduli

Mkuu Wa Mkoaaaapicc RC Arusha aagiza kusakwa waliofanya vurugu mkutano wa DC Monduli

Wed, 29 Sep 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wananchi waliojichukulia sheria mkononi wilayani Monduli na kufanya uharibifu wa kuvunja vioo vya gari la mkuu wa Wilaya ya Monduli.

Watu hao pia walivamia baadhi ya makazi ya wananchi wenzao na kufanya uharibifu wa mali.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Mongela amesema watu hao wanapaswa kuchukuliwa hatua mara moja kwani wao ni wahalifu kama walivyo wahalifu wengine na haiwezekani wao wajichukulie sheria mkononi badala ya kufuata sheria na kanuni zilizopo.

Amesema kwa mujibu wa sheria hata kama una malalamiko hupaswi kujichukulia sheria mkononi kwani hakuna mtu yeyote aliyeko juu ya sheria, hivyo watu wote wanapaswa kufuata sheria hata kama kuna tatizo gani sheria itaamua.

"Unajua tusipowashughulikia hawa watu wanaojichukulia sheria mkononi, tusipolisimamia hili iko siku watapigana na kusababisha mauaji kwani itakuwa ni mazoea, wanatakiwa wasubiri sheria ichukue mkondo wake kwani hata RC mwenyewe hayupo juu ya sheria,"amesema Mongela.

Tukio hilo limetokea Septemba 24, 2021 wilayani Monduli baada ya Mkuu wa Wilaya, Frank Mwaisumbe kumsimamisha uongozi Mwenyekiti wa kijiji Cha Engaroji na mtendaji wake kwa madai ya kutokusoma taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi Cha miaka sita.

Chanzo: mwananchidigital