Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RAS Arusha afariki dunia

2b22131283335fecf2b0efad29df2c1e RAS Arusha afariki dunia

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIBU Tawala Mkoa wa Arusha ( RAS), Richard Kwitega, amefariki dunia jana alasiri mkoani Manyara baada ya kupata ajali akienda Dodoma kikazi. Taarifa ya kifo hicho imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Kimanta.

Kimanta alisema Kwitega aliaga dunia saa 9:50 katika kituo cha afya Magugu wakati akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari. “Katibu Tawala wetu alikuwa anakwenda Dodoma kikazi na alipofika maeneo ya Mdoli gari yake iligongana uso kwa uso na basi la Makala lililokuwa linatoka Babati”alisema Kimanta.

Alisema, baada ya ajali Kwitega alipelekwa kwenye kituo cha afya cha Magugu ili baadaye apelekwe Babati kwa matibabu zaidi. Alisema kifo cha kiongozi huyo ni msiba mkubwa kwa mkoa wa Arusha hivyo ameomba wananchi wawe wavumilivu, na washikamane.

Awali jana asubuhi, Kwitega alifungua semina ya wahariri wa vyombo vya habari kuhusu mfumo wa ukusanyaji mapato ya serikali (GePG)iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mpingo jijini Arusha.

Kwitega aliteuliwa na Rais John Magufuli kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Aprili 25,2016 na kabla ya uteuzi huo aliwahi kufanyakazi katika mikoa mbalimbali.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyosainiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, Serikali pamoja na kutoa pole imesema itaendelea kuenzi mchango wa Kwitega katika ujenzi wa Taifa. Aidha taarifa hiyo ilisema taratibu za mazishi zitaendelea kutolewa na uongozi wa mkoa wa Arusha.

Chanzo: habarileo.co.tz