Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Qwihaya yaisaidia polisi kukabiliana na corona

Qwuhay ED.webp Qwihaya yaisaidia polisi kukabiliana na corona

Thu, 14 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMPUNI inayozalisha nguzo za umeme ya Qwihaya General Enterprise Co Ltd, imetoa msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kwa jeshi la polisi mjini Mafinga wilayani Mufindi.

Akikabidhi msaada huo, Meneja wa kiwanda hicho, Ntibwa Mjema amesema kuwa kampuni hiyo imeamua kushiriki vita vinavyoendelea dhidi ya corona kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na ugonjwa huo.

Mjema amesema msaada huo ni mwendelezo wa ziara ya kampuni hiyo katika ugawaji wa vifaa hivyo kwa maeneo mbalimbali na mpaka sasa tayari zaidi ya shilingi milioni 65 zimetumika kwa kazi hiyo tangu janga hilo kuanza.

“Tumetoa vitakasa mikono, barakoa na sabuni kwa askari ili wanapotekeleza majukumu yao wawe kwenye mazingira salama” amesema Mjema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Abichi Masanga, ameishukuru kampuni hiyo na kuziomba kampuni nyingizi ziige mfano huo.

“Tunashukuru kwa huu msaada na bado tunahitaji msaada mwingine, hapa wanakuja raia wengi na watuhumiwa wakiwa hapa wanahitaji barakoa na sanitaiza kwa hiyo, mahitaji makubwa yanahitajika” amesema Kamanda Masanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live