Baada ya kuwepo kwa taarifa za kampuni mbili tofauti ambazo ni Q net na Global Alliance kudhaniwa kuwatapeli wananchi hasa vijana kwa kuwadanganya kuwa wanatoa ajira huku wananchi hao wakitakiwa kutoa fedha ili wapate ajira, Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe Wilman Kapenjama Ndile amezikagua kampuni hizo na amesitisha shughuli ambazo zinatolewa na kampuni hizo huku sababu zikiwa makampuni hayo kukosa kibali na nyaraka halali za kufanya shughuli hiyo.
Baada ya kuwepo kwa taarifa za kampuni mbili tofauti ambazo ni Q net na Global Alliance kudhaniwa kuwatapeli wananchi hasa vijana kwa kuwadanganya kuwa wanatoa ajira huku wananchi hao wakitakiwa kutoa fedha ili wapate ajira, Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe Wilman Kapenjama Ndile amezikagua kampuni hizo na amesitisha shughuli ambazo zinatolewa na kampuni hizo huku sababu zikiwa makampuni hayo kukosa kibali na nyaraka halali za kufanya shughuli hiyo. Kwa upande wao baadhi ya vijana ambao wanadhaniwa kutapeliwa fedha zao na kudanganywa kuwa watapata ajira wamesema walidanganywa kuwa watapata ajira lakini baada ya kufika wamekuta vitu tofauti.