Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pwani yakabiliwa na upungufu mkubwa wa Damu

MMG 9186 Pwani yakabiliwa na upungufu mkubwa wa Damu

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkoa wa Pwani umetajwa kuwa na uhitaji wa damu salama kwa wastani wa chupa 45 kwa siku ambapo tofauti na hivi sasa ambapo unalazimika kutumia jumla ya chupa 38 pekee kiasi ambacho hakitoshelezi kulingana na uhitaji wa wagonjwa wenye uhitaji wa damu hali inayopelekea wagonjwa wengi kupatiwa rufaa nje mkoa huo kwenda hospitali ya taifa muhimbili ili kuokoa maisha.

Hayo yamebainishwa na mganga mkuu wa mkoa Gunini Kamba alipokua akizungumza wakati wa zoezi la uchangiaji damu ambalo limefanyika kimkoa wilayani Kibaha mkoani Pwani

Amesema kutokana na changamoto za ukosefu wa damu wagonjwa wengi wanaofika katika hospitali ya mkoa hulazimika kupatiwa rufaa kwenda hospitali nyinginezo ikwemo hospitali ya taifa Muhimbili hivyo akawaomba watanzania kujijengea tabia ya kuchangia damu mara kwa mara ili kusaidia wenye uhitaji ambao wengi wao wanatajwa kuwa ni akina mama wajawazito na majeruhi wa ajali wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.

Mratibu wa damu salama mkoa Pwani Denis Kapinga ameeleza kuwa mkoa umekua ukihudumia mikoa mingi ikiwamo Morogoro na Dar es salaam hivyo uhitaji wa damu umekua ukiongezeka kila wakati kutokana na ajali za mara kwa mara zinazotokea katika ukanda huo wakiwemo wajawazito waliombioni kufanyiwa upasuaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live